JK awa ahidi watanzania uchaguzi mzuri

Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai ICC Jaji Silvia Alejandra Fernandes de Gurmendi alipotembelea makao makuu ya mahakama hiyo jijini.
Rais jakaya kikwete amewaahidi watanzania wanaoishi nje ya nchi kuwa uchaguzi mkuu ujao utasimamiwa vizuri ili watanzania wapate nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka. Uchaguzi mkuu kwa mwaka huu unatarajia kufanyika wiki ya mwisho ya mwezi oktoba.
Akiwa mjini  mjhe Hague, Uholanzi Rais Kikwete  amewaeleza  watanzania hao juhudi mbalimbali za maendeleo ambazo amezifanya wakati wa utawala wake, zikiwemo ujenzi wa barabara, uboreshaji wa elimu na huduma za afya kukuza uchumi  pamoja  na nchi kujiletea maendeleo.
Mwakilishi wa  Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Uholanzi-Tane wamemueleza Rais Kikwete  katika risala yao iliyosomwa na  Johannes  Rwanzo, kuwa wangependa serikali ijayo iendeleze na kudumisha juhudi za kuimarisha uchumi.
Ameyataja baadhi ya mambo ambayo yanahitajika kuendelezwa na serikali ya awamu ijayo kuwa ni pamoja na juhudi za kupambana na umasikini nchini na ujenzi wa miundombinu.
Rais Kikwete aliyekuwemo nchini humo  amemaliza ziara yake katika Nchi za Finland, Sweden na Uholanzi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: