Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu anatarajia kufanya mkutano wa hadhara mkoani Singida mwishoni mwa wiki akijitayarisha kwenda makao makuu ya CCM kuchukua fomu ya kugombea Urais kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi juni 8.Kwa mujibu wa taarifa aliyoitoa kwa waandishi wa Habari Nyalandu amebainisha kuwa baada ya kuhutubia mkutano wake huo wa hadhara, atakwenda mjini Dodoma kuchukua rasmi fomu ya urais siku ya Jumatatu, Juni 8.Nyalandu ni mmoja wa mawaziri watakao ungana na wenzake akiwemo John Magufuri, Steven Wassira Mark Mwandosya katika Serikali ya awamu ya nne ambao wanatakaridhaa ya chama cha Mapinduzikuteuliwa kugombea urais mwaka 2015.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment