Katika hali ya kawaida watu ambao wamefikia katika hatua ya kufunga ndoa na wapenzi wao hujitahidi kufanya siku hiyokuwa ya kipekee ili kufanya sikuhiyo kuwa tofauti na siku zingine.Kuna baadhi ya watu hutumia gharama kubwa wakiamini kuwa siku hiyi ni ya kipekee na huenda isijirudie tena ambapo hutumia magari ya kifahari, farasi, na mavazi ya thamani.Katika hali ya kushangaza bibi harusi Jenny Buckleff, nchini Marekani, ameamua kushangaza umati wa watu sikuya ndoa yake baada ya kwenda ukumbini akiwa ndani ya jenezaakiwa na lengo la kuifanya siku yake kuwa ya kipekee.Hali hiyo ilimshangaza pia mume wake Christopher Lockett, ambaye hakuamini kama mke wake angeweza kufanya kitu kama hicho baada ya kuwasili ukumbini akiwa ndani ya jeneza ambalo lilikuwalikivutwa na pikipiki.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment