Nkurunziza aahirisha Uchaguzi wa Rais na Wabunge

Serikali ya Burundi imetangaza kuwa uchaguzi wa rais na wabunge uliotarajiwa kufanyika Ijumaa hii umehairishwa mpakatarehe nyingine itakapopangwa.Msemaji wa rais Nkurunzinza,Wily Nyamitwe amesema  kuwa tarehe itapangwa na wasimamizi wa uchaguzi wa nchi hiyo.Mabadiliko hayo yamekuja kutokana na taifa hilo kuingia kwenye machafuko tangu Rais Piere Nkurunzinza kutangaza nia ya kuongoza kwa awamu ya tatu baada ya kuwa rais kwa miaka 10.Umoja wa Mataifa imeelezea jinsi mgogoro huo ulivyoongezaidadi ya wakimbizi wanaoikimbia Burundi na kukimbilia nchini Tanzania.Hata hivyo umoja wa Afrika mashariki unadaiwa kushindwa kutoa amri dhidi ya Rais Nurunziza kutokana na kutaka kujiongezea muda wa kukaa madarakani kinyume  na katiba ya nchi hiyo suala linalopingwa vikali na wananchi wa nchi hiyo.

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: