Askofu wa Kanisa la Anglikana Jimbo la Dar es Salaam, Dk Valentino Mokiwa, amesema kazi ya uandikishaji wa daftari la kudumu la Wapigakura liwe endelevu kwa sababu kila siku watu wenye sifa ya kuandikishwa wanaongezeka.Hayo ameyasema jijini Dar es Salaam, wakati wa maandalizi ya maadhimisho ya miaka 50 yakuanzishwa kwa Dayosisi ya Kanisa la Anglikana yatakayofanyika Julai 5, mwaka huu kutokana na kupokea taarifa za uvunjikaji wa ndoa kwa kigezo cha BVR.Amedai kuwa endapo Serikali itafanya kazi hiyo kuwa endelevu, itasaidia kunusuru uvunjifu wa ndoa kwa sababu kazi hiyo imeonekana kuwa moja ya sababu ya wanandoa kuchelewa kurudi nyumbani kwa sababu ya foleni ya kwenyevituo vya uandikishiaji.Amedai kuwa familia nyingi zimekuwa katika mifarakano kisingizio kikubwa kikiwa ni foleninkutokana na zoezi hilo kwenye polepole jambo ambalomimechoche andoa nyingi kuvunjika na zingine wanandoakutengana.Askofu huyo ameitaka Serikali iongeze mashine za BVR na kuzihakiki ubora wake kabla ya hazijaanza kutumika ili kupunguza kero inayotokea katika familia nyingi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment