Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta leo ametangaza rasmi nia yake kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. mbele ya mamia ya wakazi wa kata ya Itetemia, Tabora mjini na wilaya za jirani na mji wa Tabora.Akizungumza na mamia ya wananchi waliofurika katika kata ya Itetemia Samweli Sitta ametaja sababu tano zilizomfanya atangaze nia yake ambazo ni:-1.MuunganoToka pande zetu mbili za muungano zinatolewa kauli na pia vitendo vyenye kuashiria nchi zetu zilizomo katika muungano yaani Tanganyika naZanzibar zitengane. Kutoka Zanzibar, tunashuhudia wanasiasa wanaodai kuwa Zanzibar itanufaika zaidi ikiwa nje ya muungano na kuwa na uhuru kamili kama nchi. Na kutoka bara tunasikia.1.Mchakato wa katibaPamoja na kuwa na muafaka kamili kuhusu katiba mpya haujapatikana, lakini katiba inayopendekezwa ina maeneo mengi ya msingi ambayo yanaweza kutuleta karibu ikiwa ni hatua ya awali inayotuwezesha kusonga mbele kwa amani.Binafsi naamini kuwa pande zinazosigana kuhusu katiba zina wazalendo ambao wanaweza kukubaliana kuwa nakipindi cha mpito cha utulivu namaelewano kitakachotuwezesha kama taifa kusonga mbele. Viongozi a kijamii na ki saisa washawishiwe kukubali hoja mbili.3.Mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwandaIli kukuza uchumi wa nchi kwa kasi inayopunguza umasiikini kwa haraka na huku tukijenga uwezo mkubwa zaidi wa bajeti ya aserikali kutosheleza huduma za ubora wa huduma za jamii kama vile afya , elimu na maji,hatuna budi kufanya jitihada za makusudi za kuubadili mfumo wa uendeshajiuwe ni wa motisha kwa wazalisha mali. Mifumo ya nchi zilizopiga hatua za maendeleo duniani ni ile iliyoweka mazingira chanya ya kuaminiana baina ya serikali na sekta binafsi. Hali hii haijatimia hapa kwetu.4.Mikakati ya dhati ya kupambana na rushwaRushwa kubwa zimekuwa na athari mbaya sana kwa uchumi wa nchi yetu. Mikataba mibovu ya huduma na mauzo, manunuzi hewa, manunuzi yaliyojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hata rushwa katika ajira, vimesababisha hasara ya matrilioni ya shilingi kwa taifa. Uchumi unakosa afya kutokana na kubanwa na rushwa ambayosasa imeenea mpaka vijijini.5 .Kuimarisha CCM kiuchumiChama tawala madhubuti ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma zote kwa ufanisi zilizoahidiwa kwenye ilani. Katika hili ni wajibu wa mwenyekiti wa chama kuhakikisha kwamba vitengo navitega uchumi vya chama vinakuwa na tija inayokiwezesha chama kuendesha shughuli zake kwa kujitegemea badala ya kutegemea ruzuku toka serikalini.Chama tawala kinachojitegemea ki uchumi ni kinga dhidi ya rushwa kwa sababu itazuia mazoea yaliyopoya wafanyabiashara wasio waaminifu kujijenga kwa mwanya wa kuwa ni “wafadhili”
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment