Viongozi wa Afrika Mashariki wametoa wito kuwa uchaguzi wa Burundi uahirishwe kwa angalau wiki sita ili mgogoro umalizike.Taarifa hiyo inafuatia mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki jijini Dar es Salaam, ambapo Rais Pierre Nkurunziza amemtuma mwakilishi wake waziri wa mambo ya Nje kuhudhuria mkutano huo hata hivyo mkutano huo haujazungumzia kugombea kwa Rais Nkurunziza.Uamuzi wa Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu wa uongozi katika uchaguzi wa mwezi ujao, umesababisha maandamano kwa majuma kadha sasa pamoja na watu kadhaa kupoteza maisha.Huenda Rais Nkurunziza ameshindwa kuhudhuria kufuatia jaribio la Mapinduzi alipohudhuria mkutano kama huo mwezi May.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment