Watu 29 wameuawa jimbo la Borno Maiduguri Kaskazini Mashariki mwa Nigeria baada ya mlipuaji wa kujitoa mhanga kujilipua ndani ya msikiti.Kamishna wa polisi katika jimbo la Borno amesema kuwa watu wengine 28 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.Shambulizi hilo lilifuatia jaribio la awali la kuuteka ya mji wa Maiduguri lilifanywa na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram. Wanagamabo haowalifyatua makombora kwenye makazi ya watu na kuua takriban watu 13.Rais Buhari Siku ya ijumaa rais mpya wa Nigeria Muhammadu Buhari aliahidi wakati wa kuapishwa kwake kuwa atakabiliana na kundi la wapiganaji wa Boko Haram na kuahidi kuwekwa kituo cha kijeshi kitawekwa katika mji wa Maiduguri kusadia kupigana na wanamgambo hao.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment