
Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao, akizungumza katika uzinduzi huo.

Mwakilishi wa Masuala ya na Biashara wa China nchini Tanzania, Lin
Zhiyong, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa vifaa mbalimbali na
viyoyozi (AC), vinavyosambazwa na Kampuni ya Midea ya china uliofanyika
Hoteli ya Hyatt Recency Dar es Salaam The Kilimanjaro leo asubuhi.

Mwakilishi wa Masuala ya na Biashara wa China nchini Tanzania, Lin
Zhiyong (katikati), akiwa meza kuu na viongozi wenzake. Kutoka kulia ni
Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen, Meneja wa Afrika wa Midea
RAC na Vifaa vya Nyumbani, Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International
Co.Ltd, Kelvin Zhao na Meneja Masoko, Peck Zhao.

Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.

Mshereheshaji wa uzinduzi huo akiongoza hafla hiyo.

Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen (kulia), akiteta jambo na Meneja Masoko, Peck Zhao.

Warembo waliokuwa wakitoa huduma ya kupokea wageni katika uzinduzi huo. Kulia ni Rebecca Paulah na Jacky Laswai.

Raia wa China wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Raia wa China wakiwa kwenye uzinduzi huo

Wadau wakiwa kwenye uzinduzi huo.

Mkurugenzi Mkuu wa Changchun International Co.Ltd, Kelvin Zhao, akizungumza na wanahabari.

Mratibu
wa uzinduzi huo, Anna Irengo (kulia), akizungumza na wanahabari.
KAMPUNI Midea ya China inayotengeneza viyoyozi (AC) imetoa ajira kwa
watanzania wapatoa 30 tangu ianze kufanya shughuli zake nchini. Hayo
yalibainishwa na Meneja wa Afrika wa Midea CAC, Tomsong Chen, wakati
akizungumza na waandishi wa habari na wadau wengine wakati wa hafla fupi
ya kuzindua viyoyozi hivyo iliyofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.
Alisema ili kuingia katika soko la ushindani kampuni hiyo imejidhatiti
kutoa huduma bora hasa katika kipindi hiki ambacho dunia ipo katika
ukuaji wa teknolojia na uharibifu wa mazingira ambapo viyoyozi hivyo
wanavyovisambaza vinasaidia kutunza mazingira. “Mbali na kukua kwa
teknolojia, vile vile tumeamua kuwekeza Tanzania ili kutoa ajira kwa
watanzania na kuwanusuru na uharibifu wa mazingira kutokana na
mabadiliko ya tabia nchi,” alisema. Chen alisema, viyoyozi hivyo
vitauzwa kwa bei nafuu ili kumpa fursa kila mtu kuweza kununua na ni kwa
matumizi ya ofisini na nyumbani. “Viyoyozi ambavyo ni kwa matumizi ya
nyumbani havitumii umeme mwingi, hivyo ni matumaini yetu tutawezesha
wananchi wengi kuvitumia,” alisema. Alisema viyoyozi vya ofisini vipo
vya ukubwa mbalimbali ambapo vingine ni kwa ajili ya matumizi ya kwenye
majengo makubwa. Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Changchun International
Co.Ltd, Kelvin Zhao, aliwataka watanzania kuzingatia kuwa viyoyozi hivyo
ni vya ubora wa hali ya juu licha ya kuwepo kwa dhana potofu ya uduni
wa bidhaa kutoka nchini China. Alitumia fursa hiyo kuwaomba wananchi na
wadau wengine kununua viyoyozi hivyo kwani ni rafiki wa mazingira.Na
Dotto Mwaibale
SOURCE. Kilimanjaro Official Blog
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment