
Ofisa
Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Jafarri
Malema (kushoto), akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo
(hawapo pichani), Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli
zinazofanywa na Rita na umuhimu wa cheti cha kuzaliwa. Kulia ni Ofisa
Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi.

Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi akizungumza katika mkutano na wafanyakazi wa gazeti la Jambo Leo.

Wafanyakazi
wa gazeti la Jambo Leo wakiwasikiliza maofisa wa Rita walipokuwa
wakizungumza nao.WANANCHI wametakiwa kuwa na vyeti vya kuzaliwa kwani
vina umuhimu katika maisha ya kila siku ndani na nje ya nchi.Mwito huo
umetolewa na Ofisa Uhusiano wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini
(RITA), Jafarri Malema wakati akizungumza na wafanyakazi wa gazeti la
Jambo Leo Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu shughuli zinazofanywa na
Rita na umuhimu wa kuwa na cheti cha kuzaliwa. "Cheti za kuzaliwa ni
msingi wa mafanikio ya kila mmoja wetu na ni muhimu kuwa nacho" alisema
Malema.Alisema Rita imekuwa ikifanya shughuli za usajili wa vizazi,vyeti
vya kuzaliwa, kuandika wosia, kusajili ndoa na talaka na udhamini kama
mali za umma na ile isiyokuwa na mwenyewe.Alisema faida ya kuandika
wosia unasaidia kuepusha watoto, mke au mume kunyang'anywa mali pale
kinapotokea kifo na inawezesha kumchagua msimamizi wa mirathi.Alitaja
faida nyingine ya kuandika wosia kuwa ni kuepusha migongano katika
familia, ndugu au jamaa na kuwa unampa uhakika wa maisha bora ya baadae
warithi wa mali waliziachiwa.Alisema jambo linalofanyika baada ya
kufariki kwa mtu aliyeandika wosia mmoja wa mashahidi anatakiwa kwenda
kutoa taarifa Rita ambapo taratibu za wosia kuwasilishwa mahali husika
hufanyika.Naye Ofisa Uhusiano wa Rita, Grace Kyasi alisema umuhimu wa
kuwa na cheti cha kuzaliwa ni mkubwa kwani ni nyaraka pekee yenye
mamlaka kisheria kuthibitisha tarehe na mahali mtu alipozaliwa na ni
nyaraka muhimu kwa kila mwananchi kwani hutumika kupata huduma nyingine
za msingi kama elimu, afya na makazi.Alisema cheti cha kuzaliwa
kinawawezesha watoto kujiunga na elimu ya msingi na sekondari na
kuwawezesha kupata nafasi ya masomo ya elimu ya juu pamoja na mikopo ya
masomo.Na Dotto Mwaibale
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment