Mwanamuziki na kiongozi wa Yamoto bendi, Aslay Isihaka, amedai kuwa ameamua kumuweka wazi mpenzi wake kutokana na kukwepa usumbufu ambao amekuwa akiupata kutoka kwa wanawake wengi kumtaka kimapenzi.Amesema kuwa kwa kufanya hivyo anahisi kama atakuwa huru na mambo yake kutokana na kero ambazo zinamfanya akose amani na mambo yake na ndio maana akaamua umma ujue kuwa ana mpenzi wake.Katika hatua nyingine amekanusha uvumi wa kuwa kimahusiano na mwanadada Wema Sepetu, na kudai kuwa huo ni uvumi tu na ndio maana ameamua kuweka wazi wapi moyo wake umelala kwa sasa ilikukwepa tuhuma hizo.Amesema kuwa watu wanaweza kuamua kuzusha ili mradi wapate cha kuongea na kudai kuwa Wema, ni kama dada yake na wanaheshimiana sana na kutaka umma kutambua kuwa ana mpenzi wake na kuacha kuzusha mambo yasiyo na ukweli.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment