WENYEVITI wa vijiji vyote 77 vya wilaya ya Ludewa mkoani Njombe wametoa tathimini yao ya utendaji wa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe na kumhakikishia ushindi wa kishindo uchaguzi mkuu utakaofanyika Octoba mwaka huu na kuomba chama cha mapinduzi (CCM) kuwaeleza wanachama wake wanaotaka ubunge kuelezwa wazi kuwa nafasi hiyo imejaa.Wenyeviti hao ambao baadhi yao ni wale waliotokana na vyama vya upinzani walitoa kauli hiyo jana wakati wa semina ya ujasiliamali iliyoandaliwa na mbunge huyo kwa wenyeviji wote 77 na watendaji wote wa serikali za vijiji 77 na kufanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Ludewa .Akizungumza kwa niaba ya wenyeviti hao Bw Andrew Mwafute alisema kuwa jitihada zilizofanywa na mbunge Filikunjombe katika wilaya ya Ludewa ni kubwa na kila mwananchi wa Ludewa na wasio wa Ludewa ambao wanafika wilayani humo ni mashahidi wa maendeleo ya sasa ya wilaya hiyo wanatambua mchango mkubwawa mbunge huyo katika maendeleo hivyo hawana sababu ya kutafuta mbunge zaidi nje ya Filikunjombe kwa sasa na kama ingekubalika waowasingehitaji uchaguzi wa mbunge .." Sisi wenyeviti wa vijiji ambao ni wawakilishi wa wananchi pamoja na watendaji wa vijiji tunatamka wazi kuwa utendaji kazi wetu umekua rahisi zaidi katika wilaya ya Ludewa kutokana na kazi kubwa inayofanywa na mbunge wetu..... mbunge Filikunjombe katika kila kijiji mradi wowote wa maendeleo kuna mchango wake wa asilimia kama si 70 basi 90 hivyo sisi tunapata faraja zaidi katika kutekeleza miradi hiyo na wananchi kutowachosha na michango "Bw Mwafute alisema kwa kazi iliyofanywa na mbunge huyo katika jimbo la Ludewa kwa kipindi cha miaka 5 ni kubwa zaidi na imezidi hata ile ya wabunge waliokaa madarakani zaidi ya miaka 40 bila kufanya kazi kubwa kama hiyo ya mbunge wa Ludewa.Hata hivyo alisema ili Ludewa izidi kusonga mbele zaidi hakuna sababu ya wana Ludewa kufanya siasa kama ilivyo maeneo mengine siasa zakuvutana kwenye mambo ya maendeleo kwani kufanya hivyo ni kujikwamisha zaidi katika maendeleo na kuwa lazima CCM kuwa na zoezi la kuwatathimini wabunge,madiwani wao na kama wamefanya kazi chini ya kiwango wakimaliza kipindi kimoja wasiruhusiwe kupewa fomu tena ila waliofanya vizuri ndio waruhusiwe kuwa wagombea pekee ndani ya chama .Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Luana Bw David Luoga alisema kwa mfano katika kijiji chake kazi zilizofanywa na mbunge huyo ni kubwa zaidi na kwa kawaida wananchi wake ni wenye msimamo wa kutochagua mbunge ama diwani kwa kipindi cha pili kama ameshindwa kutatua kero zao ila wao kwa upande wa mbunge hawahitaji mwana CCM mwingine zaidi ya mbunge wao.Alisema kamwe hawatamsahaumbunge huyo kwani ameweza kuwaharakishia maendeleo ya kijiji hicho kwa kufikisha umeme na kuwatengenezea barabara hiyo ya Malatu - Itungi ambayo ilikuwa haipitiki japo inaelekea katika taasisi mbali mbali kama nyumba za ibada, soko, Zahanati na shule ila serikali ya wilaya haikuona sababu ya kuitengeneza hadi wananchi hao walivyoomba kwa mbunge huyo katika mkutano wao wa hadhara uliofanyika miezi mitatu iliyopita .Bw Luoga alisema toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 kijiji hicho hawajapata barabaranzuri kama hiyo iliyojengwa na mbunge wao umbali wa kilomita2 iliyogharimu kiasi cha zaidi yaTsh milioni 54 barabara muhimu ambayo haikupewa umuhimu wowote na serikali ya wilaya ya Ludewa.Hivyo alisea ahsante yao kwa mbunge wao kwa kuwaletea maendeleo ni kuona wanamchagua kwa kura nyingizaidi ili kuendelea kuwa mbunge kwa vipindi vingine 15 ama zaidi na kuwa kipimo chake kilikuwa ni miaka mitano hii ambayo ameonyeha ufaulu wa zaidi ya asilimia 100 hivyo kama kijiji wananchi wameweza kuchangishana na kupata kiasi cha Tsh 100,000 kwa ajili ya kwenda kuchukulia fomu muda wa kufanya hivyo utakapofika.Pia waliomba utaratibu ulioanzishwa na mbunge huyo wa kuwakutanisha mwenyeviti na watendaji wote wa vijiji pamoja kama hivyo uendelee na miaka mingine badala ya kuwaacha wenyeviti peke yao huku madiwani wakiwa na baraza lao na kukutana mara kwa mara wakati msimamizi mkuu wa maendeleo kijijini ni wao na sio madiwani .Kwa upande wake mbunge Filkunjombe pamoja na kuwapongeza wenyeviti hao kwa kumpa faraja zaidi bado alisema wenye mamlaka ya yeye kuendelea kuwatumikia ama kutowatumikia ni wananchi wenyewe na hadi sasa bado ubunge anautamani na lengo kubwa kuzidi kuleta maendeleo zaidi ya hayo katika wilaya ya Ludewa na kueleza moja kati ya sababu ya kujivunia kuendelea kuwa mbunge ni ile ya kutekeleza ahadi zake zote alizopata kutoa kwa wananchi wakati wakampeni mwaka 2010.Alisema wananchi wa Ludewa bila kujali itikadi zao wamekuwa bega kwa bega kushirikiana katika shughuli za kimaendeleo na kupongeza pia wenyeviti wa vijiji na watendaji kwa kujitoa kwa nguvu zote kusimamia miradi ya kimaendeleo .Aidha mbunge huyo alimuagiza mkurugenzi mtendajiwa Halmashauri ya Ludewa iwapo ataendelea kuwa mbunge wa Ludewa kumuandalia kusanyiko la wenyeviti hao na watendaji kila baada ya miaka miwili japo kwa mara moja ili kubadilishana mawazo .Mwisho.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment