WANANCHI WA NJOMBE WAPATA WAKATI MGUMU BAADA YA MAMBOMUYA POLISI KURINDIMA

Wakazi wa Mji wa Njombe, jana walikumbwa na taharuki kutokana na mabomu ya machozi yaliyopigwa na Polisi kwa lengo la kutawanya waandamanaji waliokuwa wanapinga mauaji ya mkazi mmoja anayedaiwa kupigwa risasi na askari na mwingine kujeruhiwa.Hata hivyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe,Franco Kibonaalisema jana kuwa hawezi kuzungumzia tuhuma hizo wakati hali ya kiusalama haijatulia.Kamanda Kibona aliyekuwa eneo la tukio, aliwasihi wananchi kutulia kwani madai yao yanashughulikiwa.Mauaji hayo yaliyotokea juzi usiku wakati wakazi hao wawili walipokuwa kwenye klabu ya pombe ya Nyondo, Mtaa wa Kambarage.Wakazi wa eneo hilo walisema kuwa aliyeuawa ni Basil Ngole na majeruhi ni Fred Sanga ambaye amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Njombe.Wakazi hao walikusanyika hospitalini hapo saa moja asubuhi, huku wakipaza sauti zakulitaka Jeshi la Polisi kugharamia mazishi ya marehemu pamoja na matibabu ya majeruhi.Kutokana na kadhia hiyo, polisi walifika eneo la tukio na kuwatawanya waandamanaji kwa mabomu na kusababisha mmoja ambaye ni dereva wa bodaboda kujeruhiwa.Kitendo hicho kiliamsha hasira kwa wananchi ambao waliziba barabara, kwa mawe, na kuchoma magurudumu ya gari.Majeruhi Sanga akizungumza kwa tabu akiwa hospitalini alisema wakati akiwa katika klabu hiyo, askari wa doria ambao walikuwa hawajavaa sare walifika eneo hilo na kuwaweka wateja chini ya ulinzi.Alisema hali hiyo ilizua mzozo, ndipo walipolazimika kufyatua risasi ambazo zilimpata yeye namwenzake aliyefariki dunia.Mkazi mmoja wa Njombe,Emanuel Filangalialisema kitendo cha baadhi ya polisi kutumia nguvu dhidi ya raia ni cha kulaaniwa.Alisema kuwa inadaiwa kosa la marehemu na majeruhi ni kunywa pombe nje ya muda katika klabu hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: