29May2015MAUAJI YA KINYAMA BUKOBA, WAWILI WAUAWA NA KUNYOFOLEWA PUA

Kijana Joseph Gabrielanayefanya vibarua mbalimbali vya kujiingizia kipato amekutwa amekufa baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali na huku sehemu ya pua ikiwa imeondolewa sambamba na sehemu ya shavu lake la kushoto.Mwili wa Joseph Gabriel ukiwa barabarani kusubiri jeshi la polisi waje kuuondoaMauaji haya ya kutisha yametokea katika maeneo ya kata Karabagaine katika kijiji cha Kitwe.Polisi pia walichelewakufika eneo la tukio kutokana nakuwa katika eneo jingine ambako pia kulikuwa na tukio jingine la kutisha kama hili lilitokea siku moja kabla ya hili.Mwanamkemmoja ambaye jina halikuweza kufahamika mara moja, amekutwa amekufa kwa kuchinjwa shingo na pua yake kuondolewa.Pua yake ilipatikana baadae karibu na eneo la tukio.Mama huyu amekutwa na mauti katika mtaa wa Kibeta kata ya Kibeta ambapo baadaye polisi waliweza kufika na kuchukua mwili wa marehemu.Mabaki ya damu baada ya mwiliwa mwanamke kuondolewa na polisiMwezi uliopita, polisi Kagera ilitoa taarifa kwa waandishi wa habari kuhusu mauaji ya manispaa ya Bukoba, ikieleza kuwashikilia watu kadhaa na kinara wa mauaji hayo, ambao majina yamehifadhiwa kwasababu za kiusalama, huku ikisema kuwa watu wawili waliuawa na polisi kwa kupigwa risasi, wakati wakiwapeleka kwenye maeneo wanakopangia uhalifu huko Bugabo halmashauri ya Bukoba.chanzo:jamii forum
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: