WAZEE LUDEWA WAENDELEA KUMCHANGIA FILIKUNJOMBE FEDHA ZA KUCHUKULIA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE

Wazee wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameendelea kumchangia mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo.Filikunjombe fedha kwajili ya kuchukua fomu ya kugombea ubunge ili kuendelea kuliongoza jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi lilikuwa nyuma kimaendeelo.Akikabidhi fedha hizo kiasi cha shilingi elfu hamsini kwa niaba ya mzee wa kijiji cha Mbwila anayejulikana kwa jina la Mwanawalifa alisema kuwa wilaya ya Ludewa imekuwa na tabia ya kubadirisha wabunge kila inapofika kipindi cha uchaguzi kutokana na kutoridhishwa na utendaji wa wabunge hao lakini kwa sasa wameridhika na utendaji wa Filikunjombe hivyo hawaoni sababu ya kubadiri uongozi.Mzee Mwanawalifa alisema lutokana na utendaji kazi ukiambatana na umakini wa mbunge wao wazee wa kata ya Luana wameona ni vyema kumuunga mkono Filikunjombe kwa kumchangia kiasi kidogo cha fedha ili wakati ukifika achanganye na fedha zake akachukue fomu ya kugombea ubunge kwani wananchi wa jimbo la Ludewa hawana haja ya kuwa na Mbunge mwingine zaidi ya Filikunjombe.Alisema kuwa chama cha mapinduzi kimekuwa na viongozi wenye uchungu na nchiyao ambao ni waadirifu na wanaokubalika na wananchi hivyo aliwataka vijana wanaojiunga na vyama vingine kubaki njia kuu ili kuweza kugombea nafasi mbalimbali ambazo wataweza kuzitumia vyema kama Filikunjombe ambaye ni mfano wa kuigwa kwa vijana na wabunge wengine.“sisi wazee wa kijiji cha Mbwila kata ya Luana limeridhishwa na uchapakazi wako kwani maendeleo tunayaona kwa macho yetu,tulikuwa tunasikia tu katika mikoa mingine kuwa kuna maendeleo lakini leo Ludewa kunafunguka kutokana na jitihada zako hivyo tunatoa kiasi hiki kidogo ili kukuunga mkono katika kuliongoza jimbo la Ludewa tunaomba uwaeleze na vijana wenzio wa wilaya hii wanao ishi mjini kurudi na kufanya maendeleo nyumbani kama wewe”,alisema Mzee Mwanawalifa.Mzee Mwanawalifa alisema kuwa wazee wanasikitishwa sana na baadhi ya vijana waliolowea mijini bila kukumbuka nyumbani na kuiendeleza miji yaw engine haliambayo inakuwa mbaya wakati wanapofariki na kurudishwa makwao kukiwa hali mbaya hivyo alimuomba Filikunjombe kuwakumbusha vijana hao kurudi nyumbani na kufanya maendelo ili kuikomboa wilaya ya Ludewa katika wimbi la umaskini.Aidha katika ziara hiyo ya kijiji cha Mbwila Filikunjombe aliweza kutoa bati miamoja katika ujenzi wa nyumba ya Katekista katisa katoliki Mbwila na bati miamoja tena katika ujenzi wa kanisa la Anglikana Mbwila hali ambayo imewafanya wananchi wa kijiji hicho kushukuru pia kwa kuwaletea mradi wa maji.Akitoa hotuba yake Filikunjombealisema kuwa kijiji hicho kina bahati ya kuwa na maradi mkubwa wa maji lakini jitihada zinafanyika kuwaletea umeme wananchi wa kijiji hicho ambao wanashauku kubwa ya kuwa na nishati hiyo ambayo imeshafika katika kijiji cha jirani cha Luana.Filikunjombe aliwashukuru wazee wa Mbwila kwa kitendo cha kumchangia fedha za kuchukua fomu ya kugombea ubunge kwa mara ya pili alisema kuwa anashukuru kwa kuona wananchi wanatambua mchango wake wa maendeleo katika wilaya ya Ludewa kwani ni faraja iliyoje unapoona wananchi wanatambua juhudi zako za kimaendeleo.Mwisho. @habari ludewa blog
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: