LIGI YA WILAYA MTOANO MZUNGUKO WA PILI YAENDELEA WILAYANI LUDEWA KATIKA MKOA WA NJOMBE.

Ligi ya mtoano wilaya ya Ludewa Mzunguko wa pili imeanza rasmi jioni ya leo mei 13 / 2015 majira ya saa kumi kamili katika viwanja vya michezo Ludewa Mjini dhidi ya timu ya kijiji cha Maholong'wa na Timu kutoka katika kijiji Cha Luana katika kata ya Luana wilayani Ludewa. Hadi filimbi ya mwamuzi ya dakika 45 ya kipindi cha kwanza inapulizwa uwanjani hapo Maholong'wa Fc ilikuwa Nyuma kwa bao moja kwa bila bao ambalo liliwaacha hoi mashabiki waliosafiri na timu yao kutoka kijiji cha Maholong'wa hadi kufika Ludewa mjini ilikuweza kushuhudia mtanange huo ambao ni wa mtoano. Dakika 45 kipindi cha kwanza timu zotembili zilikuwa mapumziko na baadae kurejea tena uwanjani na kuanza kushambuliana kila timu ikionesha upinzani katika lango la timu pinzani huku Maholong'wa Fc ikijaribu kubadilika na kuzidi kulishambulia zaidi lango la timu ya Luana Fc. Baada ya vuta nikuvute ya muda mrefu kwa timu zote mbili mnamo dakika ya 37 ya mchezo mchezaji wa timu ya Maholong'wa Fc Aliyefahamika kwa jina la Rasta aliweza kuutumia vizuri mpira wa kona iliyopingwa na mchezaji wa timu yake baada ya kupiga kichwa cha maana na kuweza kuipa goli la kuisawazishia timu yake na kuwaacha wachezaji wa timu ya Luana wakiwa wameshikwa na butwaa kwakuwa hawakuweza kuamini kilichotokea katika uwanja huo wa michezo. Baada ya goli hilo la kusawazisha kila timu ikaanza kucheza kwa juhudi zote ili iweze kupata bao angalau moja tu la ushindi kwakuwa ligi hiyo ni ya mtoano hivyo juhudi za timu ya Maholong'wa Fc ziliweza kuzaa matunda baada ya shuti kali la moja kwa moja la mchezaji wa timu hiyo Bw, Frenk Kifaru kumshinda mlinda mlango wa timu ya Luana fc na kujikuta akifungwa goli bila mategemeo mnamo dakika ya 62 ya mchezo. Hadi Dakika 90 zinaisha Luana hawakuweza kurudisha bao hilo kutokana na mwamuzi wa mchezo huo kutoa Dakika 4 za ntongeza Luana waliweza kushambulia lango la timu ya Maholong'wa FC na kuweza kufanikiwa kusawazisha bao hilo kwa mara nyingine na kila timu kubaki na mtihani mkubwa wa kutafuta bao lingine la ushindi. Hadi filimbi ya Mwisho ya mwamuzi inapingwa uwanjani hapo kila timu ilikuwa na mabao mawili mawili hali ambayo ilimfanya mwamuzi wa mchezo huo kuamuru kupigwa kwa mikwaju ya Penalti kwakuwa ligi hiyo ni ya mtoano hivyo ilikuwa nilazima apatikane mshindi. Baada ya kupiga mikwaju hiyo ya Penalti timu ya Maholong'wa FC ILIWEZA kuchukua ushindi kwa kuilaza Timu ya Luana FC kwa mikwaju ya penalti 5--3 hivyo Maholong'wa fc waliweza kujipatia ushindi huo mnono kabisa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: