mkazi wa kijji cha Lupanga akilia kwa furaha baada ya mbnge wao Filikunjombe kuwasaidia kitanda cha kujifungulia wakati awali walikuwa hawana |
mbunge wa ludewa deo filikunjombe wa pili kushoto akisaidiana na wananchi wake kushusha bati na saruji kwa ajili ya kijiji cha lupanga |
wanafunzi wa shule ya msingi lupanga wakitoa zawadi mbali mbali kwa mbunge filikunjombe baada ya kujitolea kufanya ukarabati wa shule yao |
Filikunjombe akitazama vifaa mbali mbali vya ujenzi alivyovitoa kijiji cha Lupanga |
wananchi wakitoa zawadi ya mbuzi kwa mbunge wao |
mbunge filikunjombe akionyesha darubini aliyoitoa msaada kijiji cha lupanga kwa ajili ya zahanati |
mbunge filikunjombe akipongezwa kwa msaada wa kitanda cha kujifungulia wajawazito |
mbunge Filikunjombe akikabidhi jezi |
wanahabari joyce na deo nyoni wakifuatilia mkutano wa mbunge |
katibu mwenezi wa ccm mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya akizungumza na wananchi wa Lupanga |
diwani wa Lupanga akifurahia jambo |
Filikunjombe akiwashukuru wananchi wake |
wananchi wakimpongeza mbunge wao kwa misaada mbali mbali |
wananchi wakifurahi na mbunge wao |
mkazi wa Lupanga akitembelea magoti kama sehemu ya ahsante kwa mbunge |
Filikunjombe akisalimiana na watoto wa shule ya Lupanga |
barnabas njenjema, Ludewa
ALIYEKUWA
mbunge wa sita toka nchi ipate uhuru katika jimbo la Ludewa
Stanley Kolimba amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe kwa utendaji kazi wake na kuwa mbali ya kuwa amepata
kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo kwa nafasi ya ubunge ila
hakuweza kufanya mambo makubwa kama yanayofanywa na mbunge wa sasa
katika jimbo hilo.
Kolimba
alitoa kauli hiyo jana wakati akimshukuru mbunge Filikunjombe kwa
kusaidi vifaa mbali mbali vya ujenzi vyenye thamani ya zaidi ya Tsh
milioni 10 katika kijiji cha Lupanga kata ya Lupanga wilaya ya
Ludewa .
Alisema
jimbo hilo la Ludewa limepata kuwa na wabunge saba hadi sasa
toka nchi ipate uhuru wake mwaka 1961 ila kazi kubwa
inayofanywa na mbunge huyo wa awamu ya saba Bw Filikunjombe hakuna
mbunge ambae amepata kuifanya na kuwa kuna haja ya wananchi wa
wilaya ya Ludewa na viongozi kumpongeza mbunge huyo kwa utendaji
kazi na uwakilishi wa wananchi uliotukuka.
"kweli
kwenye ukweli tuseme kweli mimi bila shaka mnanifahamu vizuri
kuwa mwaka 2001 nilikuwa mbunge wa jimbo hili la Ludewa na
kweli kama vitu nilifanya ikiwa ni pamoja na kupeleka umeme
Ludewa mjini na kuna siku katika kuhamasisha maendeleo nilipata
kukabidhi mbuzi mmoja ila lazima niwe mkweli kasi hii ya
Filikunjombe katika kuwaletea maendeleo ni kubwa sana ukilinganisha
na sisi wabunge wote tuliopita ...sio kama nampigia debe ila ndio
ukweli wenyewe"
Hata
hivyo Kolimba ambae ni mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa
alisema heshima kubwa ya wananchi wa Ludewa kwa sasa imeanza
kuonekana kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa na mbunge huyo na
kuwa nguvu ya chama tawala .
Katibu
mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honolatus Mgaya na katibu wa CCM
wilaya ya Ludewa Lusiana Mbosa walieleza kufurahishwa na jitihada za
mbunge huyo katika kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo na kuwa
utendaji kazi wake unakiwezesha chama chao kuwa na nguvu ukilinganisha
na majimbo mengine ambayo wapinzani wameendelea kujisogeza .
Bw
Mgaya alisema mkoa wa Njombe una wabunge wengi ila heshima CCM
inavyopata Ludewa ni kubwa zaidi na iwapo wabunge wote wangefanya
kazi kama mbunge wa Ludewa hata wapinzani kuweka bendera zao
katika mkoa wa Njombe ingekuwa vigumu .
Huku
katibu wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Mbosa akiwataka wananchi wa
Ludewa katika kuendelea kukiunga mkono chama cha mapinduzi ni kupuuza
kauli za wapinzani ambao wapo kwa ajili ya kukwamisha maendeleo
kwa kupinga kila jema linalofanywa na CCM .
Alisema
kuwa wapinzani katika kuonyesha mapungufu yao na kuwa si watu wa
kuleta maendeleo ni pale walipoamua kususa bunge la katiba huku siku
zote walionyesha kupigania katiba mpya kuwa kitendo hicho ni
kuonyesha kutapenda nchi itawalike na hivyo kuwataka wananchi
kuwapuuza kwa kutowasikiliza na pindi muda utakapofika basi kuipigia
katiba inayopendekezwa kura ya ndio .
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe aliwataka wananchi hao kuendelea
kumpa ushirikiano zaidi ili kuweza kuwatumikia na kuwa kuongeza
kuwa lengo lake kuona posho anazozipata bungeni kama mbunge
zinawanufaisha wananchi wake na sivinginevyo .
Alisema
kuwa moja ya ndoto yake katika kuwatumikia wana Ludewa imetimia
hivyo kazi kubwa ya wananchi wa jimbo hilo ni kuendelea kumtumia
zaidi ili kwa upande wake kuwasaidia pale ambapo wananchi hao
wanashindwa .
katika
ziara hiyo mbunge Filikunjombe aliweza kutimiza ahadi yake ya mabati
mabati 170, saruji mifuko 200 ,kitanda cha kujifungulia wajawazito
na darubini vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya milioni 15.