KUHUSU WATOTO WATATU KUKUTWA WAMEJIFICHA KWENYE CHASIS YA BASI WAKISAFIRI KWENDA ARUSHA KUTOKA KAHAMA



Moja ya story kubwa kuripotiwa na kituo cha ITV jioni hii ni ishu ya watoto watatu wa kiume kukutwa wakiwa wamejificha kwenye chasis ya basi.

Watoto hao wamekutwa Singida ambapo tayari walikuwa wamesafiri kutoka Kahama na walikuwa wakielekea Arusha.

Watoto hao wamesema walitolewa na mtu mmoja Arusha kwenda Kahama akawaambia kuna kazi, walipofika Kahama akawatelekeza, baadae wakaamua kurudi kwa njia hiyo ya kujificha kwenye chasis ya basi.

Kamanda wa Polisi Singida ACP Thobias Sedoyeka amesema watoto hao walikutwa wakati wakaguzi wa mabasi walipokuwa wakikagua basi hilo la Mgamba Express ambapo mpaka wanafika hapo basi lilikuwa limesafiri kwa zaidi ya Kilometa 360.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: