Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ametoa ya moyoni kwamba kifo cha Kapteni Komba ni pigo kubwa kwa cha Chama Mapinduzi (CCM) wasanii pamoja na wananchi.
Akizungumza na Mtandao wa Hivisasa Waziri Membe amesema kwamba Kapt Komba ni mtu aliye jitoa muhanga kusaidia chama chake cha mapinduzi katika mbio zake zote za ushindi hivyo kuondoka kwake ni dhahiri pengo hilo halitazibika.
Aidha ,Waziri Membe amewataka wasanii kuyaenzi yale aliyotuachia hususani kwa utunzi wa nyimbo nzuri za kuelimisha jamii ya Watanzania.
Kwa upande mwingine, Mwili wa Kapt John Komba umesafirishwa kwenda Songea Mkoani Ruvuma ambapo atazikwa kijiji kwake Lituhi wilayani Nyasa tarehe 3 ambayo ni kesho.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment