Mkuchika: Watanzania wamechoshwa na wizi fedha umma

Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora George Mkuchika amesema kwamba imefikia hatua watanzania wamechoshwa kusikia upotevu wa mabilioni ya fedha za umma unaofanywa na watendaji wachache kwa manufaa yao. Wizi wa fedha hizo unatokana na rushwa unaofanywa na baadhi ya viongozi na watumishi wa umma wa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA). Inadaiwa kuwa watu wamekuwa wakivusha mizigo mikubwa bila kulipa kodi huku wakidanganya kuwa ni malighafi na pengine kuuzwa nje ya nchi. Akizungumza na watendaji wa mamlaka ya mapato Tanzania, Takukuru na viongozi wa dini katika kikao cha mpango mkakati wa TRA kupambana na rushwa George Mkuchika amesema kwamba imefikia wakati watendaji wa TRA wafanye kazi kwa kufuata maadili ya utumishi ya umma. Imebainika kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania imekuwa ikilalamikiwa sana na wananchi kuhusu kushamili kwa rushwa suala linalotakiwa kufanyiwa kazi mamlaka hiyo. Kwa upande wake kamishina mkuu wa mamlaka ya mapato nchini Bw. Rishedi bade amesema kwamba mikakati inafanyika katika kukabiliana na rushwa kwa kushirikisha wadau katika kuandaa mikakati hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: