Rais wa Shrikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF Bw. Jamal Malinzi ametuma salama za pongezi kwa Rais Boubacar Diara wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) kwa kutwaa Ubingwa wa Afrika kwa vijana U17.
Katika salam zake Malinzi amesema mafanikio mazuri waliyoyapata FMF yametokana na uongozi bora, kamati ya utendaji na mipango thabiti waliyoiweka katika soka la Vijana.
Kwa kutwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17, Mali wamepata nafasi ya kuliwakilisha Bara la Afrika kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile pamoja na nchi za Afrika Kusini,Guinea na Nigeria.
Mali wametwaa Ubingwa wa vijana Afrika U17 baada ya kuifunga timu ya taifa ya vijana ya Afrika Kusini (Amajimbo’s) kwa mabao 2-0.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu, Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), watanzania wanawapa pongezi Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Mali (FMF) wa kutwaa Ubingwa huo.
Aidha Rais Malizi pia ametuma salam za pongezi kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Afrika Kusini (SAFA) Bw. Dany Jordaan kwa timu ya Amajimbo’s kushika nafasi ya pili.
Amajimbo’s ndio timu pekee kusini mwa Bara la Afrika watakaowaklisha kwenye fainali za U17 za Dunia nchini Chile.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment