Rais Jakaya kikwete ametema chehe mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi Albino kwa kuwatangazia wanaojiuhusisha hayo kwamba serikali inatarajia itachukua hatua kali dhidi yao. Akizungumza na wananchi kwa njia ya vyombo vya habari usiku huu rais Jakaya Kikwete amesema kwamba mauaji dhidi ya watu wenye ulemavu wa Ngozi Albino ni dhahiri yanalifedhehsha taifa letu na kuturudisha kule kulikotoka. Ameongeza kuwa Albino ni wenzetu, hawapaswi kuishi kwa hofu katika mtaa, kijiji pamoja na nchi yao. Na kusisitiza kuwa jamii nzima ina wajibu wa kuhakikisha kuwa usalama wa maisha ya alabino katika maeneo wanayoishi. Akizungumzia takwimu za majuaji hayo nchini Tanzania amesema kwamba tukio la kwanza lilitokea april 17, 2006, mwaka 2008 watu 18 waliuawa, 2010 lilikuwa tukio 1, 2011 hakukuwa na tukio, 2014 waliuawa 3 na mwaka huu tukio moja limetoka Geita. Watuhumia 139 wametiwa nguvuni na mashauri 35 yamefunguliwa mahakamani, watuhumiwa 73 wameachiwa, 15 wamepatikana na hatia na watuhumiwa 13 wamehukumiwa kifo huku watuhumiwa 2 wamepata kifungo cha miezi sita. Kwa asilimia kubwa matukio ya mauji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yametokea ukanda wa ziwa huku chanzo kikubwa kikiwa ni imani za kishirikina kwa baadhi ya watu wanao daiwa kuwa ni wavuvi na wachimbaji wa madini wakiamini kuwa hawawezi kufanikiwa kwa njia za kawaida suala ambalo halina ukweli wowote. Katika hatua nyingine Rais Kikwete amewataka wananchi kuwafichua wanaofanya vitendo vya mauaji ya Albino, wanunuzi na waganga wanaochochea albino mao wakamatwe ili hatua kali za kisheria zichuliwe dhidi yao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: