Prof. Jay alaani mauaji ya Albino

Mkongwe katika muziki wa Hip-hop nchini Tanzania, Joseph Haule ‘Prof. Jay’, amelaani mauaji yanayoendelea ya walemavu wa ngozi na kuitaka serikali pamoja na wananchi kuweza kuungana kwa pamoja kuhakikisha wanatokomeza mauaji hayo. Akihojiwa amesema kuwa ni unyama uliokithiri ambapo unyama huo unapingwa na kila binadamu na kuongeza kuwa wasanii wapo mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanapaza sauti kuelimisha watu kuhusu unyama huo Amesema kuwa kama haitoshi wanahitaji kufika maeneo ambayo ukatili huo umezidi na sehemu ambazo matukio hayo hutokea mara kwa mara kuongea na wananchi wa sehemu hizo pamoja na kuwaelimisha kuachana na imani za kishirikina ambazo zinadaiwa kusababisha mambo ya mauaji. Aidha, amefurahishwa sana kusikia adhabu ya wale waliohusika na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kuiomba serikali kuongeza adhabu zaidi ili mtu akisikia au kuona ndio anapate kujua athari ya mauaji hayo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: