Chama Cha Demokrasia na Maendeleo ( CHADEMA) leo kimeshinda kesi dhidi ya aliyekuwa mwanachama wake Zitto Kabwe.
Mahakama kuu imeamua kuwa Chama kinaweza kuendelea na taratibu zake. Kesi hiyo ilifunguliwa na Zitto Kabwe ikiwa ni pingamizi kuzuia kikao cha Kamati Kuu CHADEMA kumjadili.
Aidha, Mwaka jana Zitto Kabwe aliweka pingamizi mahakamni kuzuia kamati kuu kutomjadili kabla shauri lake kusikilizwa na Baraza Kuu.
Alidai anataka mahakama iagize kamati kuu ya CHADEMA kutojadili suala lake mpaka baraza kuu likae kuamua rufaa yake.
Katika hatua nyingine jopo la wanasheria wa Chadema linalo ongozwa na Peter Kibatala na John Mallya linatarajia kuongea na Waandishi wa Habari muda mfupi ujao.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment