Katika hali isiyotegemewa mwalimu mmoja wa shule ya sekondari katika wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu(jina lake tunalihifadhi) amenusurika kufa baada ya kudaiwa kubugia juisi ambayo imeisha muda wake wa matumizi hali iliyomsababishia maumivu makali na kushindwa kutembea.
Mwalimu huyo alikunywa juisi hiyo inayodaiwa ku expire usiku wa kuamkia Jumamosi wiki hii baada ya kununua juisi katika duka la shule anayofanyia kazi.
Inaelezwa kuwa baada ya kunywa juisi hiyo alianza kujisikia tumbo kusokota na maumivu ya ajabu hali ambayo ilimshtua na kuanza kuwaza nini hasa kimemtokea.
Malunde1 blog imeambiwa huyo hali ya mwalimu huyo ilizidi kubadilika japokuwa alionesha hali ya kujikaza lakini baadaye alikimbizwa katika moja ya zahanati mjini Shinyanga kisha kupatiwa matibabu.
Akisimulia kisa kilichompata katika mahojiano maalum na Malunde1 blog,mwalimu huyo alisema:
“Pale shuleni kuna duka,ilikuwa usiku,nilinunua juisi aina ya MALT AZAM nikanywa baadaye nikaanza kuumwa tumbo,nikapata wasiwasi juu ya muda wake wa matumizi,Ndipo nikabaini kuwa Muda wake wa matumizi umeisha tangu Januari 31 mwaka huu”.
“Unajua lile ni duka linauzwa na mwalimu,kwa hiyo sikuwa na wasiwasi juu ya muda wa matumizi,kumbe laa!! Nimeonja joto ya jiwe maana maumivu niliyoyapata tangu jana usiku hasi leo Saa nane mchana siyo mchezo ndugu yangu".
"Kwanza nilikuwa na safari yangu kwenda Dar siku ya Jumamosi,niliamka asubuhi nikapanda gari hadi mjini Shinyanga kwa ajili ya safari ya Dar,huwezi amini tumbo lilikuwa linauma,nikaamua kuahirisha safari yangu,nikaenda nyumbani kwa rafiki yangu mjini Shinyanga,tukanunua dawa kwenye duka la madawa,lakini maumivu hayakuisha,nikawa natapika,hamu ya kula hakuna".
Baadaye mchana majira ya sita,jamaa yangu akanipeleka kwenye zahanati ya Kanisa Katoliki Ngokolo,nikachomwa sindano na kupewa dawa ndipo hali yangu ikawa nzuri",alieleza mwalimu huyo.
Kufuatia majanga yaliyomfika mwalimu huyo aliwaasa wananchi kujenga tabia ya kuangalia muda wa matumizi kwa vitu mbalimbali wanavyonunua kwenye maduka na kuacha kumwamini kila mtu kwa ajili ya usalama wa afya zao.
Mtandao huu umemshuhudia mwalimu huyo akipata matibabu katika zahanati hiyo
Na Kadama Malunde-Shinyanga
Home
Uncategories
HATARI..!! MWALIMU WA SEKONDARI ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUBUGIA JUISI ILIYOISHA MUDA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment