WAATHIRIKA WA MAAFA YA MVUA KUFUNGA BARABARA HUKO SHINYANGA, ZATAJWA KUSABABISHWA NA WANASIASA

Baadhi ya waathirika wa mvua ya Mawe katika kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamelazimika kuifunga barabara ya Isaka -Kahama na kuathiri kwa muda mawasiliano katika nchi ya Rwanda,Burundi na Uganda wakishinikiza serikali kuwagawia chakula,magodoro,branketi,mahema na shuka baada ya kunyeshewa na mvua usiku wakati vifaa vya misaada vikiwa vimefungiwa kwenye maghara hali iliyosababisha jeshi la polisi kuwatawanya wananchi kwa mabomu ya machozi na kufungua njia ili gari ziendelee na safari. Vurugu hizo zimedumu saa moja ambapo kundi la wananchi wenye hasira wakiilalamika kamati ya maafa kwa kushindwa kuwahudumia waathirika kwa wakati hali iliyosababisha waathirika wanaolala nje kunyeshewa mvua huku wakinamama wakila ani nguvu kubwa iliyoumika kutuliza ghasia zilizosababisha watoto kupotea kutokana na mabomu ya machozi yaliyotumika kutawanya wananchi waliofunga barabara. Kufuatia vurugu hizo mbunge wa jimbo la Msalala Mh.Ezekiel Maige amelazimika kufika kwenye eneo la tukio na kujionea hali halisi ambapo amewasihi wananchi kuwa watulivu wakati akifanya mipango ya kuzungumza na kamati ya maafa ili iweze kutoa vifaa vinavyolalamikiwa na vigawiwekwa walengwa. Alipotakiwa kujibu malalamiko hayo katibu wa maafa wilaya ya Kahama ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya ushetu kahama Bi.Isabela Chilumba amesema vurugu hizo zinasababishwa na wanasiasa na kwamba kamati ya maafa imeba ini kuna kundi la vijana kutoka vijiji jirani wakivizia chakula na vifaa vya misaada. Naye mkuu wa mkoa wa shinyanga Bw.Ally Nasoro Rufunga amekabidhi misaada hiyo kwa wenyeviti wa serikali za vitongoji na vijiji pamoja na kutoa fedha zaidi ya shilingi milioni nne kwa kaya 14 ambapo kila familia iliyofiwa imepatiwa kiasi cha shilingi laki tatu kama pole ya rambirambi ya serikali ya mkoa wa shinyanga na kuahidi kusaidia zaidi kadri misaada inavyopatikana. Via>>ITV
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: