KAGERA SUGAR YAIKATALIA COASTAL MKWAKWANI, SARE 2-2

COASTAL Union imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na Kagera Sugar jioni hii Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Coastal ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya sita, kupitia Suleiman Kibuta kabla ya Atupele Green kuisawazishia kagera Sugar dakika ya 52 akimalizia kona ya mkongwe George Kavilla. Coastal ikafanikiwa kuongoza tena mchezo kwa bao la Rama Salim kwa penalti dakika ya 67, kufuatiwa Kibuta kuchezewa rafu na beki wa Kagera, Ibrahim Job. Hata hivyo, kagera wakasawazisha kwa mara nyingine, mfungaji Enock Kyaruzi baada ya kazi nzuri ya Rashid mandawa dakika ya 85. Matokeo hayo yanaifanya kila timu ijiongezee pointi moja.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: