KAMANDA WA CHADEMA LUDEWA ATOA SHILINGI MILIONI MBILI KWAAJILI YA KUKIJENGA CHAMA.

Kamanda wa chama cha Demokrasia na Maendeleo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe ametoa kiasi cha shilingi milioni mbili katika ofisi ya chama hicho wilayani hapa kwaajili ya kukijenda chama hasa katika kipindi hiki cha kuhamasicha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura. Akitoa fedha hizo katika ofisi ya Chadema ya wilaya ya Ludewa Kamanda huyo ambaye alijitambulisha kwa jina la Ocol Adrian Haule alisema malengo makuu ya kutoa fedha hizo ni katika jitihada zake za kukijenga chama na kuiwezesha ofisi ya wilaya kufika katika maeneo yasiyofikika na kujaribu kuongea na wananchi kuhusiana na kujiandikisha katika daftari hilo. Hata hivyo aliwataka viongozi wa chama hicho ngazi ya wilaya kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa ili kujenga imani kwa wananchi kwani Chadema imekuwa inakubarika katika maeneo mengi ya nchi kutokana na uaminifu ikiwa na utendaji kazi usio na mashaka kwa wananchi. “Nimeamua kutoa fedha hizi kama kijana pia kamanda wa chama changu ninachokipenda ili kuijengea uwezo ofisi yetu ya wilaya ambayo bado haijajiimarisha ipasavyo kutokana na nguvu ya upinzani kwa wilayani Ludewa hivyo nawasihi makamanda wenzangu kuzitumia fedha hizi kwa malengo yaliyokusudiwa”,alisema Bw.Haule. Aidha Bw.Haule aliweza kutoa msaada wa bati 60 geji 28 katika kijiji cha Mkiu shule ya msingi Mkiu kata ya Mlangali zenye thamani ya shilingi milioni moja laki mbili na sitini elfu pia pesa ya usafirishaji wa bati hizo kiasi cha shilingi laki moja na arobaini kutoka Njombe hadi mkiu. Kutokana na shule hiyo ambayo imekuwa na uhaba wa vyumba vya madarasa na nyumba ya mwalimu alisema kuwa huo ni mchango wake yeye kama mzawa wa wilaya Ludewa hivyo aliamua kutoa kwa malengo ya kuikuza sekta ya elimu wilayani hapa. Bw.Haule ambaye ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam katika kitivo cha sayansi ya jamii aliwataka vijana wa wilaya ya Ludewa kumuunga mkono katika suala zima la kuiendeleza wilaya ya Ludewa kwani bado iko nyuma kielimu na kimaendeleo hivyo kila mwanaludewa anapaswa kuchangia maendeleo ya wilaya yake. Mawasiliano yake sim no.0758358986 au email ocolhaule@gmail.com. Mwisho.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: