WANANCHI WA KIJIJI CHA LUILO WAULALAMIKIA UONGOZI WA KIJIJI KWA KUCHANGISHA FEDHA ZA UJENZI WA ZAHANATI NA KUZITUMIA VISIVYO.

Wananchi wa kijiji cha Luilo wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe wameutupia lawama uongozi wa kijiji hicho kwa kuwachangisha fedha kiasi cha shilingi elfu tano kwa muda wa miaka mitatu kwaajili ya ujenzi wa Zahanati lakini mpaka sasa ujenzi huo haujaweza kuisha hivyo kuwafanya kuendelea kulipia gharama kubwa za matibabu katika zahanati ya kanisa. Akiongea kwa msisitizo jana mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la Agnes Ngalomba alisema kuwa katika kata ya Luilo ni yenye vijiji vitatu ni kijiji pekee cha Luilo ndicho wananchi wake wanatibiwa katika Zahanati ya kanisa Katoliki kwa gharama kubwa lakini vijiji vingine vyenye Zahanati za Serikali kumekuwa na gharama nafuu ambayo inawasaidia wananchi. Bi.Agnes alisema kuwa uongozi wa kijiji umepoteza imani kwa wananchi kwa kuchukua michango yao kila mwaka ya ujenzi wa Zahanati lakini ujenzi huo umekuwa ukisuasua kwani tofari za ujenzi wa Zahanati hiyo zilifyatuliwa na wananchi na kunabaadhi yao ni mafundi lakini cha kushangaza viongozi wamekuwa wakitoa taarifa kuwa fedha hizo hazitoshi kumalizia ujenzi. Alisema mpaka sasa tofari zipo na Zahanati imejengwa kufikia usawa wa madirisha na ujenzi huo umesimama hali inayosababisha baadhi ya kuta kuanza kubomoka hivyo kuwafanya wananchi kuamini fedha zao zimeliwa kwani hawajawahi kusomewa napato na matumizi ya ujenzi wa Zahanati hiyo tokea ianze kujengwa. “Fedha zetu tulizo zichanga wananchi zimeliwa kwani tofari tulifyatua wenyewe kwa nguvu zetu na mafundi wa kijiji tunao lakini mpaka sasa tunazidi kuchangishwa ili waendelee kula vizuri,hali ni mbaya ya kiuchumi inayotusababisha tushindwe kuzimudu gharama za matibabu kuanzia watoto wadogo hadi wajawazito tunalipia huduma ya afya tofauti na vijiji vya jirani”,alisema Bi.Agnes. Bi.Agnes alisema viongozi hao wa kijiji wamekuwa wakiahidi kila mwaka kuwa ujenzi huo utakamilika mapema ili wananchi waondokane na gharama kubwa wanazozitumia katika upatikanaji wa matibabu lakini ahadi hizo zimekuwa ni hewa kwani huongea hayo ili waweze kupata michango kwa wananchi na kuitafuna. Diwani wa kata hiyo ya Luilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Ludewa Mh.Mathei Kongo alipotakiwa kutolea ufafanuzi malalamiko hayo alisema kuwa huo ni uzushi tu wa baadhi ya wananchi kwani Serikali imeshatenga fedha kiasi cha shilingi milioni kumi kwaajili ya kukamilisha ujenzi huo ambao umekuwa ukisuasua katika kata yake kwa miaka mitatu hadi hivi sasa. Mh.Kongo alikili kuhusiana na uchangishwaji wa michango kwa wananchi ya ujenzi wa Zahanati hiyo lakini alisema michango hiyo haitoshi hata kidogo kukamilisha ujenzi huo hivyo mipango ya kata ilikuwa ni kumalizia ujenzi wa zahanati za vijiji vya pambeni na baadae kuelekeza kuvu katika Zahanati hiyo isiyokamilika kwa miaka mingi @habari ludewa blog
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: