BAO pekee la Didier Kavumbangu, limeipa Azam FC ushindi wa bao 1-0 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni ya leo.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Burundi, Kavumbangu alifunga bao hilo dakika ya 17 kwa kichwa akimalizia krosi ya beki wa kulia, Shomary Kapombe.
Kavumbangu sasa anatimiza mabao tisa katika mbio za ufungaji bora, akifuatiwa na Rashid Mandawa wa Kagera Sugar mwenye mabao saba sawa na Abasalim Chidiabele wa Stand United.
Na kwa ushindi huo, Azam FC inatimiza pointi 30 baada ya mechi 16, ikizidiwa pointi moja na vinara, Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi 15.
Yanga SC itacheza mechi yake ya 16 kesho, itakapomenyana na mahasimu wao wa jadi, Simba SC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Katika mchezo huo, refa Kennedy Mapunda aliwatoa nje kwa kadi nyekundu Richard Maranya wa JKT Ruvu na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ wa Azam FC dakika ya 59 baada ya kupigana.
Huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza Azam FC tangu imfukuze kocha wake, Mcameron, Joseph Marius Omog leo hii timu ikiongozwa na Mganda, George ‘Best’ Nsimbe.@bin zubery
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment