AT: Bado sijaona kazi ya menejimenti kwa wasanii

Mwanamuzikiwa miondoko ya mduara Ally Ramadhani ‘AT’amesema kuwa haoni kama kuna haja ya kuwa na menejimenti ikiwa meneja ndio anakuwa bosi wa mwanamuziki na sio mwanamuziki kuwa bosi wa meneja. Akizungumza na Hivisasa blog, amesema kuwa wasanii wana haki ya kulalamika kuwa wanaibiwa katika kazi kutokana na baadhi ya mameneja kuwa ndio watawala wa kazi za wasanii na hivyo wasanii kuwa watumwa wa mameneja wao. “Ni dhahiri muziki wa Tanzania, hauna heshima kama inafikia hatua mameneja wanakuwa mabosi wa wasanii haki haiwezi kutendeka kamwe na kama mtu anayefikiri anaweza kunishawishi kwa kile ambacho ninakitaka basi naweza kubadilika na kuwa na menejimenti,” alisema AT. Ameongeza kuwa ifike wakati watanzania wabadilike na kutetea haki za wasanii na sio kutengeneza njia za kuweza kudidimiza uchumi wa msanii na kuwanufaisha wengine na wasanii kubaki wakisota na njaa. Aidha, amewataka mameneja kuweza kutenda haki kwa wasanii na kukubali kuwa chini yao ili kuweza kukuza muziki ndani na nje ya nchi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: