Serikali imesitisha matumizi ya tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia leo (Machi 3, 2015) hadi kasoro zilizopo katika matumizi ya tiketi hizo zitakapoondolewa.
Uamuzi huo umetangazwa leo (Machi 3, 2015) jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mheshimiwa Juma Nkamia mbele ya viongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na benki ya CRDB.
Serikali imeamua kusitisha matumizi ya tiketi hizo kutokana na CRDB kushindwa kupambana na kudhibiti tiketi ‘feki’ ambazo zimekua zikitumiwa na mashabiki kwenye viwanja vingi hali iliyopekea timu kupata mapato hafifu kwenye baadhi ya mechi.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment