NHIF Yaongeza Madaktari Bingwa Hospitali ya Rufaa Tabora

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya -NHIF- umezindua huduma ya madaktari bingwa kutoka hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Taasisi ya Moi jijini Dar-es-Salaam na kuwapeleka katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete ikiwa ni moja ya sehemu ya kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko huo. Akizungumza katika hafla hiyo Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi NHIF Charles Kajege ameelezea juu ya kuanzishwa kwa huduma hiyo ya Madaktari bingwa katika mikoa mbalimbali nchini ambayo imelenga kusaidia kutoa huduma za matibabu kwa watanzania kulingana na mahitaji ya maeneo husika. Kwa upande wake mkuu wa Mkoa huo Ludovick Mwananzila amesema kuwa kupita fursa hiyo adhimu waliopewa na NHIF ni wakati wa wananchi kuonesha ushirikiano katika kujiunga na huduma za mfuko huo ili kuongeza tija katika kuwapatia huduma kwa kupatiwa kadi maalumu kwa malipo ya mara moja. Katika hatua nyingine Mganga mkuu wa mkoa wa Tabora Dokta Gunini Kamba ameushukuru uongozi wa NHIF kufikia hatua hiyo huku akiwataka madaktari katika hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi wake.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: