Breaking News: Basi la Majinja lagongana uso kwa uso na Lori

Ajali mbaya imetokea maeneo ya Mafinga Iringa sehemu kunaitwa Changarawe ambapo gari aina lori lilokuwa likitokea Dar kwenda Mbeya ambapo lilikuwa likikwepa shimo kubwa lililopo katikati ya barabara na kugongana na gari la abiria la Kampuni ya Majinja lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Dar. Hii ni maelezo ya trafki aliyepo hapa. Kontena la lori limelalia kabisa basi, na watu wengine wamelaliwa na wengine wameporomokea korongoni, mpaka sasa hakuna majeruhi ni maiti tu, wala hakuna mtu ambaye inadhaniwa amepona. - Kuna watoto wawili hapa, makadirio ya miaka ni mitatu na saba, lakini hawa inasemekana kwamba walirushwa korongoni kutokana na huo mgongano. - Uokoaji wa maiti na majeruhi walionasa kwenye ajali hapa eneo la tukio unazorota kutokana na ukosefu wa Gesi ya kukata basi kukosekana Mafinga. Juhudi zinafanyika ili kuweza kuokoa majeruhi pamoja na maiti. - Abiria walionusurika/majeruhi hali zao ni mbaya sana na haijulikani kama watafika Hospitali ya Makambako wakiwa wazima kwa sababu wanapumua kwa shida na wana wajeraha makubwa sana.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: