WASOMI LUDEWA WAASWA KUWA WAZALENDO.

picha ya pamoja ya viongozi wa Ludeso na wageni waalikwa

mtumbuizaji wa serekasi akionyesha mambo yake

 



Na.Barnabas njenjema.

Ludewa.

wasomi wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe wameaswa kuwa wazalendo kwa wilaya yao baada na pindi wamalizapo masomo yao katika vyuo mbalimbali hapa nchini na nje ya nchi.

Hayo yalitanabaishwa na afisa elimu wa sekondari mkoa wa Njombe Mwl.Izack Mgaya aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa njombe katika sherehe za ufunguzi wa tawi la shirika la maendeleo ludewa {LUDESO} linalojishughilisha na kuchochea maendeleo wilaya ya ludewa.

Pia aliongeza pia wanafunzi wote kusoma nakuelewa lugha mbalimbali za hapa duniani ilikujenga ushirikiano mzuri baina ya tanzania na nchi jirani.

''Nilitamani kulia machozi niliposikia wanataka kufuta kiingereza kwa shule na sekondari na vyuo iliniuma sana''alisema Bw.Mgaya.

Awali akitoa salam na risala kwa mgeni rasmi Rais wa shirika hilo Bw.Astomi Nkwera alisema shirika la LUDESO lilianzishwa rasmi mwaka 2001 chini ya Pr.Raphael Mwaliosi aliyekuwa mhadhiri wa chuo kikuu dar es salaam na baadae mbunge wa jimbo la Ludewa mwaka 2005 hadi 2015 ikijulikana kama Ludewa Wing na baadae kusajiriwa na serikali mwaka 2013_2014 na kuitwa LUDESO.

Aliongeza pia Shirika la maendeleo la Ludewa{LUDESO} linabeba kila aliye mpenda maendeleo ya Ludewa kuungana kwa pamoja katika kuibadilisha Ludewa,katika kupanua nakujiendeleza kielimu Bw.Nkwera alisema ni vyema kutumia teknologia kwa kujifunzayaliyo mema na sio mabaya.

Aidha ameongeza kuwa shughuli kubwa za shirikika la maendeleo Ludewa linajihusisha na kuelimisha wananchi juu ya katiba inayopendekezwa,kutoa elimu juu ya kujiandikisha katikadaftari la wadumu la wapiga kura,kutoa elimu kwa wajasiriamali na wakulima wadogo wadogo.

Pia hakusita kumshukuru Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe kwa juhudi zake za kujitolea kuwasaidia wananchi na shirika hilo kwa Ludewa bila ya ubaguzi  wa aina yeyeto.

Akitanabaisha maendeleo ya shirika hilo alisema kuwa kwa sasa wana ekari takribani kumi za matunda ya miparachichi kwa kuanzia ili kuendana na kasi ya maendeleo  wilayani hapa.

Akitoa salaam za shukrani mwenyekiti wa chama cha ccm Ludewa Bw.stanley kolimba amewaasa wana shirikisho hao kuto kujiusha na siasa na kufanya ivyo kutaharibu umoja huo ambao unamalengo ya kuwakomboa wana ludewa katika nyanja zote.



x

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: