Baada ya ushindi mgumu ilioupata kwenye mechi liyopita ya Ligi Kuu Tanzania Bara mbele ya JKT Ruvu, wakongwe wa ligi hiyo timu ya Simba SC itashuka uwanjani Jumamosi hii kukipiga na timu ya Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya’ kwenye uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga ikiwa ni mwendelezo wa ligi hiyo inayodhaminiwa na Vodacom.
Kocha mkuu wa Wekundu wa Msimbazi Goran Kopunovic ambae pia alikuwepo kwenye mechi ya Coastal Union walipocheza na Yanga amesema kiokosi chake kipo fiti kuwakabili Wagosi wa kaya na wanatarajia kuchomoka na point tatu muhimu kwenye mchezo huo.
“Tumejiandaa vya kutosha kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya wenyeji wetu na hatuwahofii hata kidogo, tunahitaji kushinda mchezo huo ili kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi,” Kopunovich amesema.
Simba kwa sasa inashikilia nafasi ya nane katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 16 wakati wapinzani wao wapo nafasi ya saba wakiwa wameshajikusanyia pointi 17. Wekundu wa Msimbazi wanahitaji ushindi ili wapande mpaka kwenye nafasi nne za juu kwenye msimamo wa ligi.
Msemaji wa timu ya Simba SC Humphrey Nyasio alimesema, wana malengo ya kushinda kwenye mchezo huo dhidi ya Coastal kwani kikosi chao kimeandaliwa vizuri kushinda mchezo huo wa ugenini. Lakini akawaomba wapenzi na mashabiki wa Simba kuiunga mkono timu yao kwa kuishangilia itakapokua inamenyana na wenyeji wao, kwani itawasaidia wachezaji kujiamini.
“Tutakapokua tunasaka ushindi siku ya Jumamosi, tunaomba mashabiki waishaingilie timu kwa nguvu maana itawajengea wachezaji hali ya kujiamini na kuinua ari ya wachezaji wawapo uwanjani,” Nyasio alisisitiza.
Lakini haitakua kazi rahisi kwa Simba kushinda mbele ya Coastal Union waliopoteza mchezo wao wa Jumatano dhidi ya Yanga kwa goli 1-0 wakiwa nyumbani. Matokeo hayo ya yaufanya mchezo kuwa mgumu kwani Coastal endapo watashinda mchezo huo watafikiha jumla ya pointi 20 na kupanda mpaka nafasi ya tatu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment