Azam FC: Tumevuna mengi Kongo

Azam FC: Tumevuna mengi Kongo Licha ya kutoshinda mechi hata moja katika kambi iliyoweka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), mabingwa wa soka Tanzania Bara, Azam FC wamesema ziara hiyo ilikuwa na mafanikio katika maandalizi yao ya mechi ya awali ya ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya vigogo wa Sudan, El-Merreikh. Msemaji wa Azam, Jaffar Idd amesema timu imepata wamepata mazoezi ya kutosha ukizingatia wamecheza mechi za kimataifa licha ya kutoshinda. “Tumejua makosa yetu na udhaifu wetu, kocha tayari anaendelea na marekebisho na tupo tayari kwa mechi yetu ya raundi ya kwanza dhidi ya El-Merreikh”, alisema Iddi. Azam imerejea Dar es Salaam Alhamisi ikitoka Lubumbashi na baada ya kurudi wanajiandaa na mechi kadhaa za ligi kuu ya Tanzania kama maandalizi yake ya mwisho kabla kuwavaa Wasudan. Wakiwa DRC Kongo, walicheza na mabingwa mara nne wa ligi ya mabingwa Afrika, klabu ya TP Mazembe na kufungwa 1-0. Wakatoka droo ya 2-2 na timu ya ZESCO Unitsd ya Zambia kabla ya kupoteza 1-0 mbele ya Don Bosco katika mechi yao ya mwisho. Iddi amesema wana matumaini makubwa ya kuanza vyema michuano ya kimataifa baada ya bechi lao la ufundi kuyafanyia kazi mambo kadhaa. Hii ni mara ya kwanza kwa Azam kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa Afrika na itacheza na El Merreikh ya Sudan Februari 15 jijini Dar es Salaam. Mechi ya marudiano itapigwa mjini Khartoum, Sudan baada ya wiki mbili.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: