Aliyemuua Polisi auawa na wananchi wenye hasira kali

Dodoma, Wananchi wenye hasira kali wamemuua mtuhumiwa anayejulikana kwa jina la Tissi Mallya aliyetoroka baada ya kumuua askari Polisi mwenye namba G.7168 Koplo Joseph Swai. Akizungumza na waandishi wa habari jana Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, David Misime alisema mauaji hayo yalitokea juzi asubuhi katika eneo la Chang’ombe juu ambapo Mtuhumiwa Tissi Mallya ambaye alitoroka baada ya kumuua askari Polisi ameuawa usiku wa kuamkia jana na wananchi alipokuwa amejificha akiwa na panga lenye damu, lililotumika kwenye mauaji hayo. Kamanda Misime alisema baada ya Malya kutekeleza mauaji hayo alikimbia, lakini ilipofika majira ya saa 5 usiku wananchi walimuona maeneo ya Mtimkavu Mailimbili akiwa bado na panga alilotumia kumuua Koplo Joseph. Katika hatua nyingine Kamanda Misime alisema katika kumbukumbu walizonazo ni kuwa mwaka 2006 Malya aliwahi kufungwa miaka mitatu kwa kosa la kujeruhi, pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita kwa kosa la kutishia kuua.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: