Ngasa apiga mbili, Yanga ikirejea kileleni

Timu ya Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa leo. Mrisho Ngasa aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya mshabuliaji wa Liberia Kpah Sherman ndiye aliyeibeba Yanga leo kwa kufunga mabao yote mawili. Ngasa alifunga goli la kwanza dakika ya 56 akiunganisha krosi safi iliyopigwa na Simon Msuva, na kuongeza goli la pili kwa kuitumia vizuri pasi aliyopewa na Andre Coutinho. Yanga imelipa kisasi leo kwa Mtibwa Sugar baada ya kufungwa kwenye mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. kwa matokeo hayo Yanga wanarejea kileleni mwa ligi wakiwa na pointi 25 pointi tatu mbele ya bingwa mtetezi Azam wenye pointi 22 lakini wakiwa na mchezo wa kiporo mkononi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: