Bomu limelipuka nje ya ikulu ya rais wa Yemen, katika mji mkuu, Sanaa, mji ambao sasa unadhibitiwa na wapiganaji wa madhehubu ya Shia, wa Houthi Inaarifiwa kuwa waasi wawili wa Houthi walijeruhiwa. Hapo jana wapiganaji hao walilivunja bunge kabla ya kudhibiti madaraka. Sasa wapiganaji hao wamebuni halmashauri ya usalama kuongoza nchi hadi bunge la muda litakapoundwa. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwa liko tayari kuchukua hatua zaidi, iwapo wapiganaji hao hawatarudi haraka kwenye mazungumzo, kuhusu kipindi cha mpito cha kuelekea kwenye demokrasi. Baraza jipya limewataka wapiganaji wamuachilie huru rais wa Yemen, waziri mkuu, na baraza la mawaziri kutoka kifungo cha nyumbani.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: