Mwanamuziki kutoka jumba la sanaa nchini Tanzania (THT), Mwasiti Almas, amekanusha kuwa na uhusiano na mtangazaji wa East Africa Redio, Sam Misago, muda mfupi baada ya kupokea salamu za heri ya kuzaliwa kutoka kwa mwanamuziki Naseeb Abdul “Diamond”.
Amesema kuwa baada ya kupata salamu kutoka kwa Diamond, iliyosema “Happy Birthday Chitty…muke halali ya @Sammisago” alishtuka kidogo lakini hakuna kitu kama hicho baina yake na mtangazaji huyo.
Amesema anashindwa kupata jibu la haraka tetesi hizo Diamond, amezitoa wapi kutokana na ukweli kuwa yeye bado hajaolewa na kuongeza kuwa wao ni marafiki kama walivyo wengine na wamejuana muda mrefu.
Amesema kuwa anaamini kuwa Sam, ana mchumba wake na yeye pia, ila ameshtuka sana kutokana na kupigiwa simu na watu wengi kuuliza kama kuna ukweli wowote na kuongeza kuwa hajawahi kuweka bayana mahusiano yake na ikitokea ameolewa atasema.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment