Katika hali ya kushangaza mtoto mmoja mwenye jinsia ya kike nchini China, amezua gumzo baada ya kuzaliwa akiwa na ujauzito wa mapacha.
Mtoto huyo ambaye wazazi wake wanaishi Bara la China, alizaliwa katika hospitali ya Qeen Elizabeth, ambapo alifanyiwa upasuaji baada ya wiki tatu kutoa vijusi ambavyo tayari vilikuwa na miguu, mgongo, mikono, ubavu na utumbo.
Hata hivyo viumbe hao tayari walikuwa na uzito mmoja wa gramu 14.2 na mwinginge gramu 9.3.na wote walikuwa tayari wana uti wa mgongo ambapo upasuaji ulifanyika salama na mtoto huyo aliruhusiwa kutoka hospital siku nane baadaye.
Hali ijulikanayo kama kijusi katika kijusi hutokea mara moja tu katika vizazi 500,000 duniani ambapo kesi chini ya 200 hazijawahi kutolewa taarifa.
Kwa upande wake Dkt. Yu Kai, ambaye ni mtaalamu katika masuala ya uzazi na gyneacology, anaamini kuwa hilo ndio tukio la kwanza kuwahi kutokea katika mji huo.
“Ni vigumu kugundua kijusi wakati mtoto akiwa tumboni kwa mama ambapo kijusi hicho ndani ya mtoto huwa kidogo sana kuweza kuonekana,” alisema Yu.
Amesema kuwa haiwezekani kwa msichana mdogo kwa kuwa na mimba juu ya mimba hivyo urutubishaji wa mbegu za watoto mapacha bila shaka ni mali ya wazazi wake, ambazo ilikwenda katika sehemu isiyo sahihi.
Taarifa zinasema kuwa sababu za kutokuwa sawa kwa binti huyo aliyezaliwa 2010 bado hazijafahamika na Shirika la Afya duniani limetambua kuwa ni aina moja wapo ya saratani.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment