Wafungwa watoroka baada ya demu ‘kuwadatisha’ walinzi

Wafungwa 28 wametoroka jela la Nova Mutum, karibu na Cuiaba nchini Brazil baada ya kukabiliwa na majaribu kutoka kwa wanawake waliowarubuni walinzi wakiume eti kuwapa maraha. Watoa ‘raha’ hao waliwarubuni walinzi kiasi cha kuwaacha watupu wa mnyama, kuwafunga pingu na kutoroka na silaha zao. Polisi waliwagundua walinzi hao watatu asubui yake baada ya habari kusambaa. Kwa mujibu wa upelelezi, wanawake hao waliwalewesha walinzi wale ‘wenye uchu’ kwa kuwapa whiskey iliyokuwa imewekwa madawa ya kulewesha. Polisi wamesema kuwa kati ya wanawake hao watatu, mmoja wao aliripotiwa kuwa rafiki wa kike wa mfungwa mmoja aliyetoroka ambapo alifika saa tisa Alhamis asubuhi na kuomba kuingia ndani kunywa na kuongea na mtu wake. Kwa mujibu wa Bi Angelina de Andrades Ferreira, Msemaji, baada ya kuwanywesha pombe walinzi, wanawake hao waliwafunga na pingu, wakachukua funguo na kuwafungulia wafungwa wote. Angelina, amesema mpango wa kutoroka ulipangwa na mchumba wa mmoja kati ya wanawake hao, Bruno Amorim, ambaye alikuwa akikabiliwa na tuhuma za majaribio ya mauaji, na wizi wa silaha za moto na kuongeza kuwa kila kitu kilikuwa kimepangwa na kutimizwa kwa msaada wa hao wanawake. Aidha maafisa magereza hao watatu wamewekwa chini ya ulinzi na watashtakiwa kwa kosa la kutoroka kwa wafungwa jela, uzembe, na wizi wa silaha za moto.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: