Kufuatia familia moja ya watu 6 kufariki kwa ajali ya moto katika Kata ya Kipawa, Mtaa wa Kipunguni ‘A’ jijini Dar, jeshi la Zima moto limetoa kauli kuhusiana na atukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo msemaji wa jeshi hilo, Inspekta Puyo Nzalayaimis amesema ukosefu wa taarifa kamili kuhusu eneo la ajali ya moto ambayo ilitokea Februari 7 mwaka huu na kuua watu sita wa familia ndiyo ulisababisha jeshi hilo kuchelewa kufika katika eneo hilo na kufanya uokoaji .
Aidha inadaiwa kuwa nyumba ilianza kuungua usiku ambapo jeshi lake lilifika saa 12 alfajiri na kukuta nyumba yote imeteketea na moto kuwaua watu wote waliokuwa ndani.
Katika hatua nyingine ofisa huyo aliwataka wananchi kutoa taarifa mapema ya tukio husika kwa kupiga namba ya dharura 114 ili kuliwezesha jeshi kufika kwa muda mwafaka.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment