Kipa wa Mbeya City, David Burhani amesimamishwa kwa muda usiojulikana.
Mbeya City ililala kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani Mbeya dhidi ya Yanga ambao waliwazidi ujanja na kumaliza ufalme wao wa Uwanja wa Sokoine.
Sababu tatu zilizosababisha kusimishwa kwake baada ya kikao cha mabosi wa Mbeya City jana zimebainika.
Kwanza ni bao la Mrisho Ngassa aliyefunga baada ya kumpokonya mpira na kupachika mpira wavuni kuandika bao la pili.
Pili ni kushindwa kuzitokea krosi, ikionekana katika mechi hiyo makosa yalifanana hadi alipofungwa bao la kichwa la Simon Msuva.
Katika mechi hiyo, pia imeonekana kulikuwa na makosa mengi yaliyofanana na mechi tatu zilizopita na lionywa kabla.
Kutokana na hali hiyo, City wakaamua kumsimamisha Burhan, hata hivyo haijaelezwa kama waliwasiliana na Kocha Mkuu, Juma Mwambusi kuthibitisha hayo.
Burhan amekuwa kipa tegemeo wa City na aliiwezesha kufanya vema msimu uliopita.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment