HAYAWI HAYAWI... MATOKEO YA KIDATO CHA NNE YAMEKAMILIKA... KUWA WA KWANZA KUJUA

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema usahihishaji wa mitihani ya kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, umekamilika. Katibu mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema kuwa“usahihishaji umekamilika na baraza lipo katika uchambuzi wa kuyapanga na tutakapokamilisha tutayatangaza”. Alipoulizwa ni lini hasa matokeo hayo yatatangazwa, Dk Msonde alisema: “Tumemaliza kusahihisha na mchakato wa kuyapanga ukikamilika tutawaeleza hivyo msiwe na shaka.” Kikawaida matokeo hutoka mwishoni mwa mwezi wa pili.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: