Na MatukiodaimaBlog
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amewataka viongozi wa kisiasa kuweza kujitafakari juu ya nafasi wanazoziongoza ili kuona kama wapo kwa ajili yao binafsi ama kwa ajili ya jamii iliyowachagua.
Filikunjombe alitoa kauli hiyo jana wakati akitoa salam zake za pore kwa wakazi wa Ludewa katika mazishi ya aliyekuwa mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa (NEC) wilayani hapo Elizabeth Haule yaliyofanyika kijijini kwake Luana , kuwa lazima viongozi kujenga utamaduni wa kuwatumikia wananchi ambao wamewawezesha kuwa na nafasi hizo badala ya kujinufaisha wao.
Mbunge Filikunjombe alisema kuwa wilaya ya Ludewa imempoteza kiongozi imara na kuwa uongozi wa MNEC huyo ulikuwa ni wa kuigwa kutokana na namna ambavyo alivyokuwa akiwasilisha mambo yake na siku zote kuonyesha kuwatumikia wana CCM waliomuwezesha kuwa MNEC.
" Siku mbili kabla ya kifo chake nilipata kuzungumza na marehemu kupanga juu ya sherehe ya CCM ila alinikumbusha juu ya barabara ya Malato ,Itundu alikuja kwangu na kuniomba kila wakati .....hadi siku ya mwisho nikipangana nae mwishoni aliniuliza ahadi yake juu ya barabara vipi na siku moja nilimtania kuwa wewe ni mkazi wa Malato na unasali Anglicana na ile barabara inakwenda kanisa la Roman Katoliki ila alisema wote ni watu wake ....hivyo naomba nisema siwezi kuacha kutekeleza ombi lake la barabara"
Mbunge huyo alisema kuwa amepata kujifunza mengi kutoka kwa marehemu huyo enzi za uhai alikuwa akiomba pasipo kutumia nguvu na moja kati ya jambo ambalo alikuwa akimuomba ni pamoja na kusaidia kuchonga barabara ya kijiji hicho kuelekea kanisa la RC yenye urefu wa Kilometa 3 kutoka barabara kuu ya Ludewa - Njombe itakayotumia kiasi cha Tsh milioni 26 .
" Mimi pia nimepata kujifunza kutoka kwa marehemu huyo kumbe unaweza kuomba bila kutumia nguvu zaidi na ukapata ....suala hili la kuniomba kusaidia kuchonga barabara kila wakati amekuwa akinipigia simu na kuniomba lakini naomba kutamka leo hapa kuwa nitamuenzi kwa kutengeneza barabara hiyo ambayo hakuna hata mwananchi mmoja amepata kuniomba barabara hiyo itajengwa mwezi wa sita na pia nitasogeza umeme kutoka Malato kwenda kitongoji cha Itundu kuanzia mwezi wa tano mwaka huu"
Alisema kuwa marehemu alikuwa akiutumia uongozi wake vizuri kwa kuwajali wananchi wake hivyo ni vema kila kiongozi wa kisiasa kuona anatumia vema nafasi yake aliyopewa na wananchi kwa kuwatumikia waliomchagua.
Aidha alisema kuwa kwa upande wake bungeni akiwa anaomba jambo kwa ajili ya wana Ludewa siku zote amekuwa akitumia nguvu lakini marehemu yeye alikuwa akiomba kwa unyenyekevu na siku zote alikuwa ni mtu wa kuwatumikia wananchi wake hivyo lazima kila kiongozi wa siasa kujitafakari zaidi .
Marehemu Haule katika uhai wake mbali ya kuwa mjumbe wa NEC Taifa akiwakilisha wilaya ya Ludewa pia alikuwa ni mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Ludewa na mwenyekiti wa kikundi cha Sanaa Ludewa alifariki kwa ugonjwa wa moyo juzi katika Hospitali ya wilaya ya Ludewa baada ya kuzidiwa toka jumapili akitokea katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa CCM
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment