Mkufunzi wa Kijerumani Gernot Rohr amechaguliwa na chama cha soka nchini Burkina Faso kuziba pengo lililoachwa wazi na Paul Put ambaye akufanya vyema akiwa na timu hiyo kwenye michuano ya kombe la mataifa ya Afrika iliyofanyika nchini Guinea ya Ikweta.
Chama cha soka nchini Burkina Faso kikitoa taarifa kwa vyombo vya habari usiku wa jumanne kimesema kinafurahia uteuzi huo na kitamtambulisha kwa vyombo vya habari siku za karibuni.
Kwenye kinyan’ganyiro hicho kikali kilijumuisha makocha Stephen Keshi,Milovan Rajevac na kocha aliechaguliwa Gernot Rohr. Gernot Rohr anauzoefu na soka la Afrika ambapo kabla alishafundisha nchi za Gabon na Niger.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment