Julio wa ‘Mwadui’ atua Coastal rasmi

Kocha wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ tayari ameanza rasmi mazoezi na timu ya Coastal Union ya mkoani Tanga baada ya uongozi timu hiyo kumuomba akasaidane na kocha mkuu wa timu hiyo inayoonekana kukosa mwelekeo hasa kwenye raundi ya pili ya ligi kuu Tanzania Bara. Julio ameenda kuisaidia timu ya Coastal kama sehemu ya ‘urafiki’uliopo kati yake na timu hiyo ili kuboresha benchi la ufundi la Costal Union. Coastal inayonolewa na kocha Mkenya James Nandwa imekua haina matokeo mazuri kwenye siku za usoni ndio maana Julio ameitwa kikosini hapo ili kuongeza nguvu. Julio alifanya mazungumzo na viongozi wa timu ya Coastal Union kabla ya kwenda kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga kuzungumza na wachezaji. Viongozi aliozungumza nao Julio ni pamoja na kocha mkuu wa timu hiyo James Nandwa, mjumbe wa kamati ya utendaji Albert Peter, katibu mkuu Kassim El Siagi na meneja wa Coastal Union Akida Machai
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: