MNYIKA AWATAKA WANANCHI WA LUDEWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA
Na;Barnabas njenjema
Ludewa
Naibu katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendelea amewataka wananchi wa ludewa na tanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika kujiandikisha daftari la wapiga kura pindi awamu yao itakapofika;
hayo aliyasema wakatika akihututubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa chama cha chadema uliofanyika katika viwanja vya soko wilaya ya ludewa;
hali kadhaalika naibu katibu huyo wa chadema alitumia fursa hiyo kueleza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja nasuala la mh:chenge kufikishwa mbele ya kamati ya maadili na kueleza kuwa hayo yote yanatoka na serikali kuto kutoa adhabu kwa mafisadi pindi wanaposhindwa kutimiza wajibu wao;
hakusita kusisitiza maadili kwa viongozi mbalimbali wa serika haswa katika suala la Tegeta escow account ambalo linaendelea kuitafuna nchi hasa walala hoi;
pia akijibu swali lililoulizwa na wananchi juu ya madini ya makaa ya mawe na liganga pamoja na wakulimwa kulipwa fedha zao mnyika alisema "mm kama waziri kivuli wa nishati na madin nliiomba mikataba mbalimbali ya madini nikambiwa ipo ila nikifika ofisini naambiwa ni siri;mwanzo bungeni tulikuwa tunajadili liganga na mchuchuma sasa ni gesi ya lind na mtwara"alisema mh;mnyika
halikadhalika kwa upande wa mahindi ya wakulima ambao hawajalipwa fedha zao mnyika alisema"kipindi bunge linaendelea wabunge wengi waliuza juu ya suala hilo ila majibu kutoka kwa wazari wa kilimo na chakula yalikuwa ni tayari tumewalipa na ambao bado watalipwa hivi punde kumbe bado hamjalipwa sasa tutakaporudi bungeni tutakomaa na waziri wa chakula hadi kieleweke"alisema mnyika
mbunge huyo amekuwa na ziara ya mkoa wa njombe akifanya mikutano kuhamasisha wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftar la wapiga kura ametembelea wilaya ya njombe;ludewa;makete; pamoja na vijiji vya matamba;lugarawa;wanging'ombe ili kuwapa hamasa wananchi:
pia amewaomba viongozi wengine wa siasa kufanya ivyo ili watu wajitokeze kwa wingi;
"nimeongea na tume makambako na zoezi la kuandikisha ludewa ni kuanzia tarehe16;3 ivyo mjitokeze kwa wingi katika kujiandikisha'alisema mnyika
ili kufanikisha zoezi hilo kwa chama cha chadema kufika vijiji mh:mnyika alichangisha fedha kwa ajiri ya kufanikisha hilo kwa viongozi wa ukawa wilaya ya ludewa ambapo jumla ya sh;269900 zilipatika kutoka kwa wananchi wa wilaya ya ludewa;
Home
Uncategories
MNYIKA AWATAKA WANANCHI WA LUDEWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUJIANDIKISHA DAFTARI LA WAPIGA KURA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment